Thursday, January 7, 2021

Wa Asi wa Kabila ya kifuliro wameuwa raiya wanyamulenge tena

Taarifa za habari kutoka katika kijiji kiitwacho Kuri Gongwa zinasema kuwa vijana wa kabila la Wafuliiru Biloze Bishambuke wamekivamia kijiji hicho na kukishambulia na kuua Raia kadhaa wa kabila la Wanyamulenge na kupora Ngo'ombe zisizo pungua 30 hii jioni ya leo Jumanne tarehe 6/1/2021.

Taarifa zinasema kuwa mauaji hayo na uporaji huo vimetekelezwa na vijana kutoka vijiji vya Wafuliiru vilivyo katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti na utawala wa kamanda mkuu wa Biloze Bishambuke na Maï Maï Mushombe na Kashumba ambao kwa mara nyingi wanaendelesha machafuko yakiwemo mauaji uporaji na unyanga'anyi dhidi ya Wanyamulenge waishio maeneoni humo. 

Ikumbukwe kuwa kila mara wa Maï Maï pamoja na Biloze Bishambuke hushambulia Wanyamulenge wakiwaua kupora Ngo'ombe zao ikiwemo mifugo mingine midogo na kuchoma moto Nyumba zao na baadae Wanyamulenge wakifuatilia mifugo yao ndipo wafapo raia wasiokuwa na hatia suala ambalo limewaongezea raia matatizo mazito ya kulipa damu yaho fidia kwa kosa ambalo hawakulitenda kwasababu wahalifu hao wafanyavyo hivyo huingia kwenye vijiji vya Wafuliiru nakugawana walivyopora wakisikia kuwa Wanyamulenge wanafua Ngo'ombe zao basi wa Maï Maï pamoja na Biloze Bishambuke hukimbia na kuingia porini basi na kuwasababishia raia wao matatizo mukubwa hivyo bila kujali wala kuwajibika. 

Tunatoa mwito kwa raia wa kabila la Wafuliiru Wanyindu waishio katika maeneo yanayomilikiwa na wa Maï Maï pamoja na Biloze Bishambuke kujihadhari na kutokushika Ngo'ombe ambazo zimeporwa wala kula nyama za hizo Ngo'ombe kwasababu zitawasababishia vita visivyo isha katika maeneo yao na wakemee vikali wahalifu hao wala wasifungiwe nira pamoja. 

*Ngarura Patrick*

No comments: